Local Bulletins

Mji wa Moyale wapandishwa hadhi kuwa Manispaa

Gavana wa kaunti ya Marsabit Mohamed Ali amesema kuwa kaunti ya Marsabit inazidi kupiga hatua kimaendeleo.

Akizungumza alipozindua manispaa ya Moyale, Gavana Ali amesema kuwa serikali yake inazidi kuwekeza zaidi katika masuala ya maendeleo jimboni huku akitaja hatua ya kufanya Moyale kuwa manispaa kuwa ni mfano tosha kuwa serekali inajali wananchi wake.

Huku akisifia hatua hii, Ali ameelezea kuwa uzinduzi wa manispaa ya Moyale itasaidia kuhakikisha kuwa eneo hilo limeafikia hadhi ya kibiashara ya kimataifa.

Aidha amesema kuwa Moyale imepokezwa hadhi hiyo ya umanispaa baada ya kukaguliwa na kuonekana kuwa imeafikiana na vipengele vinavyohitajika.

Gavana Ali amewashauri wanabiashara kushirikiana na serekali ya kaunti ili kuhakikisha kuwa wameboresha manispaa hiyo huku akisema kuwa atajumuisha jamii zilizo katika eneo hilo katika uongozi wa manispaa.

Mkuu huyo wa kaunti ameelezea kuwa serekali ya kaunti ya Marsabit inajizatiti kuhakikisha kuwa maeneo yanayonawiri kibiashara yamefanywa kuwa manispaa ili kuinua hadhi ya biashara katika maeneo hayo.

Subscribe to eNewsletter