Local Bulletins

Mikakati yote imekamilika kuhakikisha wanafunzi wa Grade 9 wanaendelea na masomo – Asema mkurugenzi wa elimu Marsabit Peter Magiri.

Wazazi walio na wanafunzi wanaojiunga na gredi ya tisa katika kaunti ya Marsabit wametakaiwa kutohifia chochote kwani mikakati ya kuhakikisha kwamba wanafunzi hao wanaendelea na elimu yao ipasavyo imewekwa.

Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani ofisi mwake mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri amesema kuwa serekali imehakikisha kwamba madarasa yanayofaa kutumika na wanafunzi hao yamekamilika haswa wakati huu shule zinapofunguliwa kwa muhula wa kwanza wa mwaka wa 2025.

Magiri ametaja kwamba mkumbo wa kwanza wa madarasa hayo umekamilka kwa asilimia mia huko mkumbo wa pili ukiwa katika asilimia 95 kukamilika.

Aidha Magiri ameweka wazi kuwa serekali pia amehakikisha kwamba vitabu vya kusoma vimesambazwa katika kila shule ili kuhakikisha wanafunzi hao hawatatiziki.

Hata hivyo Magiri ametoa onyo kwa wazazi ambao wamewaoza wanao wangali wachanga kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria huku akiwataka wasichana waliopata ujauzito kuruhusiwa kurejea shuleni ili kuendelea na elimu baada ya kujifungua.

 

Subscribe to eNewsletter