Local Bulletins

Mbunge Dido Raso ashutumu wanaokosoa kuondolewa kwa mchujo wa kupokezwa kitambulisho cha kitaifa.

NA JB NATELENG

Siku chache baada ya Rais William Ruto kufutilia mbali hitaji la wakazi wa kaskazini mashariki mwa nchi kufanyiwa ukaguzi kabla ya kupatiwa vitambulisho vya kitaifa viongozi wa maeneo hayo wamekumbatia agizo hilo wakisema itawafaidi katika kuhakikisha kuwa wakazi wa maeneo hayo wamepata vitambulisho.

Kiongozi wa hivi punde kukumbatia agizo hilo ni Mbunge wa Saku Ali Dido Rasso ambaye amesifia hatua hiyo na kumpongeza Rais kwa kuleta usawa kwa wananchi wa maeneo hayo.

Rasso amesema kuwa kwa miaka 60 wamekuwa wakinyimwa haki yao ya kuweza kujisajili kama wakenya na agizo hili huenda likawa ni mwamko mpya kwao na kwa vizazi vijavyo.

Huku akijibu matamshi ya gavana wa Trans Nzoia Goerge Natembeya, Rasso amesema kuwa ni wakati sahihi ambapo wafugaji wanafaa kufurahia haki yao ya kuwa wakenya akimtaka Natembea kuweza kuunga mkono agizo hili.

Subscribe to eNewsletter