Wasichana na wanawake Marsabit watakiwa kufanya kozi ya sayansi ili kuendana soko la ajira.
February 11, 2025
Na JohnBosco Nateleng
Maendeleo lazima ifikie kila mmoja katika eneo la Saku” haya ni kwa Mujibu wa Mbunge wa Saku Ali Dido Rasso.
Akizungumza alipokuwa akikabidhi shule ya upili ya Gadamoji basi pamoja na kuzindua mikakati ya miaka mitano ya shule hiyo, Rasso amedokeza kuwa lazima serekali pamoja na wahizani wawekeze katika elimu ili kuinua hadhi ya jamii pamoja na kuondoa umaskini mashinani.
Rasso amesisitiza kuwa ni wajibu wa Kila kiongozi kuhakikisha kuwa amewekeza katika kuboresha elimu jimboni.
Rasso pia amekanusha madai yaliyoibuliwa kuhusiana na basari ya eneo bunge la Saku akisema kuwa ni uwongo kwa sababu eneo lako limepiga hatua katika masuala ya Elimu..