Local Bulletins

Mahakama – Kesi ya mauaji ya watoto mapacha yaliyofanyika Marsabit hayatasuluhushwa nje ya mahakama kupitia mfumo (AJS)

Na Caroline Waforo

Kesi ya mauaji ya watoto mapacha katika eneo la Dololo, kaunti ndogo ya Dukana kaunti ya Marsabit haitasuluhushwa nje ya mahakama kupitia mfumo mbadala wa sheria maarufu Alternative Justice System.

Haya yamewekwa wazi na hakimu mwandamizi wa mahakama ya Marsabit Simon Arome.

Arome amezunguma wakati wa kikao cha kuhamasisha umma kuhusu sheria na haki kilichoandaliwa Ijumaa hii katika mahakama ya Marsabit.

Katika kikao hicho Arome pia amesema kuwa kesi za dhulma za kijinsia zimeongezeka humu jimboni Marsabit.

Ongezeko hili akisema kuwa linasababishwa na mizozo ya kinyumbani pamoja na utumizi wa mihadarati kati ya maswala mengine.

Vile vile ametoa hakikisho la haki na usawa wakati wa kusuluhisha kesi mahakamani na hata nje ya mahakama kupitia mfumo wa Aternative Justice Sytem.

Mahakama ya Marsabit inahudumia kesi mbalimbali ikiwemo za jinai ambapo amewataka wananchi kujua kuwa wana haki ya kupewa bondi pamoja na haki ya kutoa ushahidi.

Kesi nyingine zinazoshughulikiwa ni pamoja na kesi za mashamba zilizo chini ya shilingi milioni 20, kesi za watoto pamoja na kesi za kiraia ukipenda.

Wakati uo huo hakimu mwandamizi wa Mahakama ya kadhi ya Marsabit Mustafa Guyo amesema kuwa kesi za talaka zimepungua katika mahakama hiyo.

Subscribe to eNewsletter