Local Bulletins

Mafunzo ya siku tano ya waamuzi maarufu Referees katika eneo bunge la Saku yaingia siku yake ya pili hii leo.

Na Isaac Waihenya,

Mafunzo ya siku tano ya waamuzi maarufu Referees katika eneo bunge la Saku yameingia siku yake ya pili hii leo.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa kike katika shirikisho la Soka nchini FKF tawi la Marsabit Jeremiah Jattani Honey ni kuwa watu 42 wamehudhuria mafunzo hayo ikiwemo wanadada watatu katika kituo cha Marsabit Youth Empowerment Center, mjini Marsabit.

Jattani akizungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani ametaja kuwa idadi hiyo imezidi ile waliotarajia.

Aidha Jattani amepongeza ongezeko la idadi ya wanadada waliojitokeza katika mafunzo hayo huku akitoa wito kwa wanadada zaidi kukumbatia mafunzo hayo katika siku za usoni.

Baadhi ya waliohudhuria mafunzo hayo wamepongeza hatua hiyo wakiitaja kama itakayoinua viwango vya soka katika kaunti.

Wamepongeza shirikisho la soka FKF tawi la Marsabit kwa kile wamekitaja kuwa ni kuwajali na kulenga kuinua viwango vya soka hapa jimboni Marsabit.

Baadhi ya wanadada ambao pia wamehudhuria hafla hiyo wameitaja kama itakayowainua pia kitaluma huku wakitoa wito kwa wengine kuikumbatia pia.

 

Subscribe to eNewsletter