Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
NA JB NATELENG
Ni afueni kwa wafanyibiashara wa Moyale baada ya serekali ya kaunti ya Marsabit kuzindua rasmi manispaa ya Moyale.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huu, waziri wa ardhi kaunti ya Marsabit Amina challa amesema kuwa wafanyibiashara wa Moyale watakuwa na uhuru wa kufanya biashara bila shida yoyote huku akiwataka wakazi wa eneo hilo kushabikia hatua ya mji wao kupewa hadhi ya manispaa.
Amina ameelezea kuwa hatua ya kufanya Moyale kuwa Munispa ni bora Zaidi kwa sababu ya ukaribu wake na nchi jirani ya Ethiopia hivyo kuimarisha pia biashara baina ya nchi ya Kenya na Ethiopia.
Amina ameelezea kuwa wizara hiyo inaendeleza mchakato wa kupanga na kupima ardhi ili kuimarisha usalama wa umiliki wa ardhi kwa wakazi wote jimboni
Kauli yake imeungwa mkono na naibu gavana wa Marsabit Solom Gubo ambaye amesema kuwa ili kuimarisha na kuboresha manispaa hii lazima jamii zinazoishi Moyale wadumishe Amani na uelewano.