Mwanaume moja wa miaka 38 ameponea kifo baada ya jaribio la kujitoa uhai kwa kujinyonga kutibuka usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Soweto mjini Laisamis kaunti ya Marsabit.
February 7, 2025
NA CAROL WAFORO
Kijana wa miaka 16 amefariki baada ya kugongwa na lori la kusafirisha mifugo katika eneo la Laisamis kwenye barabara kuu ya Marsabit-Isiolo.
Chifu wa eneo la Laisamis Agostine Supeer amethibitisha kisa hicho kilichotokea tarehe 5 mwezi huu wa Februari.
Kulingana na Chifu Supeer kijana huyo aliyekuwa mchungaji alikuwa anaomba maji kwa wasafiri wanaotumia barabara hiyo kabla ya ajali kutokea.
Kutokana na kisa hicho Chifu Super amewataka madereva kuwa waangalifu wanapotumia barabara hiyo ili kuepuka ajali za barabarabani.
Dereva aliyehusika katika ajali hiyo alijiwasilisha katika kituo cha polisi cha Laisamis. Kijana aliyefari kitiyari amezikwa.