Wanabodaboda, Marsabit wakosoa mswaada wa sheria za bodaboda.
February 25, 2025
NA CAROLINE WAFORO
Idara ya usalama kaunti ya Marsabit inaendelea na msako dhidi ya mihadarati na pombe haramu.
Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani afisini mwake kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amesema kuwa wiki jana walifanikiwa kunasa misoko 116 ya bangi humu mjini Marsabit ambapo mshukiwa alipigwa faini ya shilingi 20,000 mahakamani.
Aidha wiki iyo hiyo walifanikiwa kunasa lita 22 za pombe haramu mjini marsabit.
Kati ya lita hizo 22 mshukiwa moja alinaswa na lita 13 na kufikishwa mhakamani ambapo alipigwa faini ya shilingi 50,000. Mshukiwa wa pili akanaswa na lita 5 na kupigwa faini ya shilingi 10,000 huku mshukiwa wa tatu akinaswa na lita 4 ambapo kesi dhidi yake inaendelea mahakamani.
Kamanda Kimaiyo amesema kuwa msako huo utaendelea huku akitoa onyo kwa walanguzi wa dawa za kulevya pamoja na wale wanaojishughulisha na biashara ya pombe haramu.
Wazazi wametakiwa kuwajibika katika malezi ya wanao na kuwaepusha kujihusisha na uendeshaji wa bodaboda humu jimboni Marsabit.
Ni wito ambao umetolewa na kamanda wa polisi katika kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo.
Matamshi ya Kimaiyo yanajiri huku wanafunzi wakitarajiwa kurejea nyumbani kwa likizo fupi ya katikati mwa muhula.