Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
Na Samuel Kosgei
Serikali kupitia idara ya usajili wa watu kaunti ya Marsabit imezindua huduma mpya ya kuandikisha wanaosaka kitambulisho katika ofisi kuu ya Huduma Centre mjini Marsabit.
Kulingana na msajili mkuu katika ofisi ya kitambulisho kaunti ya Marsabit Isaac Kibet ni kuwa huduma hiyo mpya itasaidia kurahisisha kupatikana kwa kitambulisho kwa wakaazi wa Marsabit ambao kwa muda wamekuwa wakichukua muda mrefu kupata sakabadhi hiyo muhimu.
Anasema kuwa meza hiyo iliyozinduliwa wiki hii itakuwa inatoa huduma hiyo kama ofisi kuu zote za kaunti ndogo japo sasa muda wa kupata kitambulisho hicho utakuwa siku 10 pekee ikilinganishwa na Zaidi ya mwezi mmoja siku za hapo nyuma.
Kibet amewataka wazazi kuandamana na watoto wao na naibu chifu katika ofisi ya huduma centre sasa ili kupata kitambulisho katika kipindi cha siku kumi kwani serikali imeleta huduma hiyo muhimu karibu nao.
Ofisi ya Huduma Center kwa muda imekuwa ikiwapa kitambulisho wakenya pekee waliopoteza stakabadhi hiyo muhimu.
Ameongeza kuwa tayari serikali imeondoa kikwazo cha kupigwa msasa (vetting) kwa wote wanaosaka kitambulisho baada ya rais William Ruto wiki jana alipozuru kaunti ya Mandera kutupilia mbali hitaji hilo kwa kigezo kuwa inawatenga wakenya wanaoishi mpakani.
Kauli yake hiyo imekaririwa na naibu kamishna wa Marsabit central David Saruni.