Wazee waonywa dhidi ya kusuluhisha kesi za dhulma za kijinsia vijini…
January 30, 2025
Na Caroline Waforo
Idara ya mifugo jimboni Marsabit inapanga kutoa msaada wa mifugo kwa wafugaji walioathirika zaidi na kiangazi kilichoshuhudiwa jimboni katika kipindi cha mwaka 2021 hadi mwaka 2023.
Mifugo itakayotolewa ni ngamia 400 wa kike wa kati ya miaka 3-4 watakaonufaisha wafugaji kutoka maeneo bunge yote manne.
Haya ni kulingana na kaimu Mkrugenzi wa madaktari wa mifugo jimboni Marsabit Boku Bodha aliyezungumza na shajara ya radio jangwani hapo jana Jumatano wakati wa mkutano wa kujadili majanga yanayoikuba jimbo hili.
Mpango huu ni kwa ushirikiano na mamlaka ya kudhibiti athari za ukame NDMA na utaigharimu serikali kuu milioni 42.
Kulingana na Boku familia zitakazonufaika ni kutoka kwa kundi ambalo hunufaika na msaada wa kifedha kutoka kwa mpango wa HUNGER SAFETY NET program (HSNP).
Kulingana na daktari Boku mpango huu unaotarajiwa kufanikishwa katika kipindi cha mwaka moja utawahakikishia walengwa usalama wa chakula.
Idara ya mifugo inalenga kutoa ngamia kutokana na usatahimilivu wake msimu wa kiangazi.
Katika msimu huo wa kiangazi zaidi ya asilimia 70 ya kifugo waliangamia jimboni Marsabit.