Local Bulletins

Idara ya jinsia kaunti ya Marsabit yalaani kisa cha mauaji ya watoto wawili mapacha katika eneo la Dololo,North Horr.

NA ISAAC WAIHENYA

Idara ya jinsia kaunti ya Marsabit imelaani kisa cha mauaji ya watoto wawili mapacha waliouwawa katika eneo la Dololo kaunti ndogo ya North Horr.

Kwa mujibu wa afisa mkuu katika idara ya jinsia Anna Marie Denge ni kuwa ni jambo la kuhuzunisha kuona kwamba bado kuna jamii zinaendelea mila hiyo potovu kama ya kuwaua watoto wa kwanza mapacha kuzaliwa katika familia kutokana na Imani kuwa wataletea familia ‘Nuksi’.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani ofisini mwake, Anna Maria amekitaja kitendo kama kinavuta nyumba hatua zilipigwa katika kupambana na mila potovu hapa jimboni Marsabit.

Aidha Anna Maria ameweka wazi kuwa idara ya jinsia itashirikiana na mashirika mbalimbali yasiyoyakiserekali hapa jimboni kuhakikisha kwamba hamasa inatolewa kwa wananchi haswa wa mashinani kuhusiana na kuasi mila potovu na zilizopitwa na muda.

Ametoa onyo kwa wale wanaoendeleza mila potovu na zinazowadhuri wanadamu kuwa watakuchuliwa hatua kali za kisheria.

Hata hivyo afisa huyu wa jinsia amewataka wazee wa jamii mbalimbali jimboni kuangazia upya baadhi ya jamii na kuzitupilia mbali ili kuzuia kurejelewa kwa kisa kama hicho.

Subscribe to eNewsletter