Local Bulletins

Hospitali na zahanati zote jimboni Marsabit sasa ziko na dawa. – Asema waziri wa Afya Malicha Boru…

Na JB Nateleng,

Serekali ya kaunti ya Marsabit kupitia idara ya afya imesambaza madawa katika hospitali na zahanati zote jimboni.

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, Waziri wa Afya kaunti ya Marsabit Malicha Boru ameeleza kuwa idara hiyo imesambaza kiwango cha dawa ambayo kinagharimu shilingi millioni 50 katika hospitali na zahanati mbalimbali za jimbo ili kuhakikisha kuwa sekta ya afya imeboreshwa.

Waziri Boru amesema kuwa zoezi hili ambalo lilianza wiki jana linadhamiria kuhakikisha kwamba dawa zinapatikana katika zahanati na hospitali zote Jimboni huku akiwarai wakazi kuweza kuwa na subira wakati serekali inaendeleza zoezi hilo.

Aidha waziri Boru ameweka wazi kuwa dawa zimesambazwa kulingana na hitaji la hospitali ama zahanati katika kaunti ndogo zote hapa jimboni.

Hata hivyo waziri Boru amekariri kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atayepatikana akiuza dawa ambazo ziko na nembo ya serekali katika duka la madawa.

Subscribe to eNewsletter