Idara ya Watoto Marsabit yawarai wazazi kuwarejesha wanao shuleni,muhula wa kwanza wa 2025….
January 8, 2025
Idara ya utabiri wa hali ya hewa hapa Marsabit imesema kuwa hali ya kiangazi itazidi kushuhudiwa mwezi huu
Mkurugenzi wa utabiri wa hali ya hewa kaunti ya Marsabit Abdi Dokata amesema kuwa kiangazi itaendelea kwa sasa hadi wakati utabiri utakapobadilika.
Ameshauri wananchi wa Marsabit kuepuka kutembea kwenye jua na kunywa maji mengi msimu huu ambapo nyuzi-joto ziko juu sana ikilinganishwa na miezi ya mwisho ya mwaka jana.
Kitaifa ni kwamba Hali ya hewa kwa ujumla inatarajiwa kuwa ya jua na kavu katika sehemu nyingi za nchi.
Hata hivyo, mvua nyepesi hadi ya wastani inaweza kushuhudiwa mara kwa mara katika maeneo machache ya Nyanda za Juu Magharibi na Mashariki mwa Bonde la Ufa, Ukanda wa Ziwa Victoria, Bonde la Ufa sehemu ya Kusini, Ukanda wa Pwani, na maeneo ya chini ya Kusini Mashariki.