Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
Shirikisho la soka nchini FKF tawi la Marsabit linaweka mikakati kambambe ya kuhakikisha kwamba maswala ya michezo yanaendelezwa kiutalamu na kwa mipangilio inayofaa.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa FKF tawi la Marsabit Godana Roba ni kuwa wanapanga kukutana kama washikadau mbalimbali katika sekta hiyo ili kulaini mambo pamoja na utendakazi wa shirikisho hilo.
Godana amewataka wananchi wa Marsabit kuwa subira wanapojiandaa kuhakikisha kwamba hadhi ya michezo hapa jimboni inaimarika.
Baadhi ya mambo wanayolenga ni ikiwemo mafunzo ya marefari, makocha pamoja na washikadau wengine.