Local Bulletins

FKF tawi la Marsabit kuandaa mafunzo ya Mareferee kuanzia hapo Kesho.

Na Isaac Waihenya,

Kama njia mojawapo ya kuinua viwango vya soka katika kaunti ya Marsabit, shirikisho la soka nchini FKF tawi la Marsabit linapania kutoa mafunzo kwa waamuzi wa michuano maarufu Referees.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa FKF tawi la Marsabit Godana Roba ni kuwa zoezi hilo litandaliwa katika eneo la Moyale sawa na hapa mjini Marsabit kwa wakti mmoja.

Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu,Godana amesema kwamba mafunzo haya ni mojawapo ya sehemu ya maadalizi ya kuongo’a nanga kwa ligi ya hapa jimboni Marsabit ambayo haijakuwepo tangu mwaka wa 2019.

Mafunzo hayo yanatarajhiwa kuandaliwa kuanzia tarehe 27 mwezi huu wa Februari hadi tarehe 3 mwezi ujao wa Machi.

Kando na hilo FKF Marsabit pia itaendeleza zoezi la kusajili vilabu ili kuhakikisha orodha ya vilabu vyote vitakavyoshiriki katika ligi hiyo inawekwa sawa mapema iwezekanavyo.

Kadhalika Godana ameahidi kushirikiana na serekali ya sasa ya kaunti ya Marsabit ili kuondoa migogoro yeyote inayoweza kulemaza au kudunisha kiwango cha soka hapa jimboni Marsabit.

Japo hakuweka wazi tarehe rasmi ya kuanza kwa ligi ya kaunti Marsabit, ila mkuu huyu wa FKF tawi la Marsabit ametaja kwamba huenda ikaaza hata kabla ya mwezi wa nne mwaka huu iwapo mikakati yote itakamilika mapema.

Subscribe to eNewsletter