Wazee waonywa dhidi ya kusuluhisha kesi za dhulma za kijinsia vijini…
January 30, 2025
Na caroline waforo
Huku serikali ikitarajiwa kuzindua mpango wa chanjo kwa mifugo nchini wafugaji jimboni Marsabit wameendelea kufafanuliwa kwamba chanjo hiyo sio ya lazima japo wameelezwa kuwa ina manufaa mengi.
Akizungumza na shajara ya radio jangwani kaimu mkurugenzi wa madaktari wa mifugo jimboni Marsabit Boku Bodha amesema kuwa chanjo hiyo itawawezesha wafugaji kupata soko bora kwa mifugo yao.
Serikali ya Kitaifa kupitia Idara ya Ustawi wa Mifugo ilitangaza kuanzisha mpango wa utoaji chanjo kwa ng’ombe milioni 22 kuzuia ugonjwa wa miguu na midomo (FMD) na kondoo na mbuzi milioni 50 dhidi ya ugonjwa wa (PDP).
Vilevile ametupilia mbali madai kuwa wafugaji watakao kataa mifugo wao kuchanjwa hawatapata soko la mifugo wao.