Local Bulletins

Chama cha kutetea maslahi ya walimu (KUPPET) chataka serikali kuharakisha kutoa pesa za kufadhili huduma za masomo.

Na Samuel Kosgei

Chama cha kutetea maslahi ya walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri (KUPPET) kimekariri haja ya serikali kuharakisha kutuma mgao wa pesa za kufadhili huduma za masomo.

Katibu wa chama hicho cha KUPPET tawi la Marsabit Sarr Galgalo amesema kuwa walimu wakuu tayari wameanza kuwatuma wanafunzi nyumbani kuendea karo ili waweze kufadhili shughuli za shule kutokana na serikali kuchelewa kutuma pesa kwenye akaunti zao.

Ameambia shajara kuwa muungano wa walimu wakuu kwenye warsha yao na waziri wa elimu walikubaliana kuachiliwa kwa pesa hizo mapema ili isitatize masomo muhula huu wa kwanza.

Anasema kuwa kukosekana kwa pesa hizo za serikali kunalemaza juhudi za walimu wakuu kufaulisha oparesheni za shule ikiwemo ununuzi wa vyakula na vifaa muhimu vya kufunzia.

Aidha Sarr amesema kuwa kwenye mazungumzo ya Tathmini na Maendeleo (ADC) waliyofanya mwaka jana ulielezea kuwa mkataba wa maelewano wa CBA wa mwaka 2025-2029 utawasilishwa kwenye mwajiri wao TSC kufikia mwezi wa February mwaka huu.

Wameomba pia mwajiri wao TSC kutekeleza makubaliano yao ndani CBA kwa mikumbo miwili ndani  ya miaka miwili badala ya mara nne ndani ya miaka minne.

Subscribe to eNewsletter