Viongozi Marsabit wakosoa hatua ya serekali kuvunjilia mbali shirika la NACONNET….
February 4, 2025
Na Joseph Muchai,
Bweni la shule ya upili ya Marsabit Boys limechomeka usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari ni kuwa moto huo ulichipuka kwenye bweni moja japo kufikia sasa habari kuhusiana na majeruhi haijatolewa.
Juhudi zetu za kupata taarifa kutoka kwa mwalimu mkuu ziligonga mwamba kwani aliwafurusha waandishi wa habari. Maafisa wa DCI wamechukua taarifa huku uchunguzi ukiendelea.
Inaarifiwa kuwa wakati wa tukio kanisa la shule hiyo lilivunjwa na viti 17 kuibiwa.
Tukio hilo linajiri siku chache baada ya kinanda cha kanisa la shule hiyo pamoja na vifaa vingine kuibiwa.
Ni kisa ambacho kimekemewa na muungano wa kidini pamoja na muungano wa wachungaji. Akiongea na kituo hiki mwenyekiti wa muungano wa wawachingaji iba saido amewaomba waliohusika na wizi huo kuvirejesha vifaa hivyo.