Bunge la Marsabit laidhinisha bajeti ya ziada ya sh. 233m ili kufanikisha miradi ya serikali
February 26, 2025
Na Samuel Kosgei
BUNGE la kaunti ya Marsabit hii leo limepitisha bajeti ya ziada ya shilingi milioni 233 ili kufanikisha maombi ya kifedha yaliyoagizwa na serikali yake gavana Mohamud Ali.
Mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kaunti ya Marsabit Daud Tomasot ameambia shajara kuwa bunge limepitisha bajeti hiyo ya ziada kufuatia ombi la serikali ya kaunti.
Tomasot amesema kuwa upungufu huo wa shilingi milioni 233 ulitokana na kuondolewa kwa mswada wa fedha mwaka wa 2024 na pia ili kufanikisha ulipaji wa madeni ya watu waliofanya kazi na kaunti ya Marsabit.
Anasema kuwa kupatikana kuwa pesa hizo kutafanikisha kaunti kuwalipa wakenya waliopewa kazi na hata kuendelezwa kwa miradi iliyokwama.
Katika bajeti hiyo ya ziada kamati ya bajeti imeidhinisha sh.10m kwa ajili kusaidia katika kupambana na vita dhidi ya ugonjwa wa kalazar ambao umekuwa donda sugu katika idara ya afya ya umma.
Mwakilishi wadi huyo wa Korr amesema kuwa katika Makadirio ya bajeti ya mwaka huu kwa ujumla ni shilingi 10.3bn. Hesabu hiyo anasema inajumlisha bilioni 4 za maendeleo huku matumizi ya kila mwezi ikifikia bilioni 6.