Local Bulletins

Bunge la kaunti ya Marsabit yalenga kuendeleza hatua ya kuondoa ardhi ya Karare kwenye hifadhi ya wanyama.

Na Samuel Kosgei

Mwakilishi wadi wa Karare Joseph Leruk amesema kuwa kamati ya bunge la kaunti linalenga kujadiliana na ofisi ya gavana namna ya kuwasilisha katika bunge la kitaifa mswada kuhusu kuondolewa kwa ardhi ya Karare kutoka kwa hifadhi ya mbuga ya wanyama, mswada uliopitishwa na bunge la Marsabit mwaka jana.

Akizungumza nasi ofisini mwake Leruk ambaye aliwasilisha mswada kwa niaba ya wakaazi wa Karare ameambia shajara kuwa Ijumaa hii wanalenga kumfahamisha gavana wa Marsabit Mohamud Ali kuhusu mpango huo ili apeleke mbele kama mzigo wa jimbo bali sio kama mzigo wa wakaazi wa Karare.

Anasema kuwa pindi tu hatua nzima itakapokamilika basi zoezi la kugawanya ardhi ya Karare kutoka sehemu ya hifadhi ya wanyama itaanza mara moja kupitia kutengwa kwa pesa kwenye bajeti ili kufanikisha zoezi hilo.

Mswada huo wa kuondoa ardhi hiyo kwenye hifadhi ya wanyama ilijadiliwa na bunge la kaunti na kupitishwa wiki ya mwisho mwezi wa 11 mwaka jana.

Subscribe to eNewsletter