Local Bulletins

Baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Meru wamshutumu Gachagua kwa kumdunisha naibu rais Kithure Kindiki.

Na Samuel Kosgei

BAADHI ya wakaazi wa kaunti ya Meru wameendeleza shutuma kali dhidi ya aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua wakimshutumu kwa kumradharau na kumkosea heshima naibu rais wa sasa Kithure Kindiki na rais William Ruto.

Wakizungumza katika gatuzi la Meru wakaazi hao wamesema kuwa Gachagua hakutumia miaka yake miwili kuwasaidia alipokuwa mamlakani na badala yake aliisahau mlima Kenya upande wa mashariki.

Wamesema kuwa Gachagua anafaa kuacha kuchochea wananchi na kueneza maneno ya chuki dhidi ya rais Ruto na naibu wake Kithure Kindiki.

Subscribe to eNewsletter