Idara ya Watoto Marsabit yawarai wazazi kuwarejesha wanao shuleni,muhula wa kwanza wa 2025….
January 8, 2025
Usalama umeimarika kwa kiwango kikubwa katika kaunti ndogo ya Loiyangalani hii ni baada ya vitengo vya usalama kuendesha operesheni ya kutoa hamasa kwa wakazi katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa OCPD wa eneo hilo Nicholas Mutua ni kuwa kupitia ushirikiano wa maafisa wa usalama pamoja na wakazi katika eneo hilo wameweza kutoa hamasa kuhusu umuhimu wa Amani kwa wazee pamoja na vijana ambao wanachunga mifugo katika fora jambo ambalo limesaidia katika kuleta uwiano baina ya jamii zinaoishi katika eneo hilo pamoja na jamii kutoka eneo jirani la North Horr.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, Mutua amesema kuwa biashara zimeweza kuboreshwa baada ya wakazi wa eneo hilo kuasi uhasama na badala yake kuishi Amani.
Kadhalika Mutua amewarai wakazi wa Loiyangalani kuwa makini wanapotumia moto msimu huu ambapo eneo hilo linashuhudia upepo mwingi kwani ni hatari kuacha moto bila kizima kwa sababu unaweza kuleta madhara makubwa.
Vilevile Mutua amekariri kuwa kuna haja ya wakazi wa eneo hilo kuhamasishwa kuhusiana na umuhimu wa kuripoti visa vya nyumba kuteketea moto katika kituo cha polisi ili uchunguzi ufanyike kubaini chanjo cha moto na pia mali iliyoteketea.