Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Sasa ni afueni kwa wanafunzi 132 wa shule ya upili ya Goro Rukesa katika eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit baada ya baraza la mitihani nchini KNEC kuachilia matokeo ya mitihani yao ambayo yalikuwa yameshikiliwa.
Wakati wa kutangazwa matokeo ya KCSE 2024 juma moja lililopita, ni watahiniwa saba pekee katika ya watahiniwa 139 waliokalia mtihani huo 7 katika shule hiyo waliopokea matokeo yao.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka idara ya elimu ni kuwa matokeo hayo yaliachiliwa siku ya ijumaa wiki jana baada ya baraza hilo kukamilisha uchunguzi wake uliokuwa unaendelea kubaini iwapo wanafunzi hao walihusika katika udanganyifu wa mitihani au la.
Katika matokeo hayo sasa wanafunzi 23 wamefanikiwa kujiunga na chou kikuu kutoka shuleni humo baada ya kupata alama ya C Plus kwenda juu ambapo wawili walipata alama ya B minus huku watahiniwa 21 wakipata alama ya C Plus.
Hata hivyo wanafunzi 73 wamepata alama ya C stand, 40 wakipata alama ya C minus na watatu wakizoa alama ya D plus.