Local Bulletins

Wakazi wa Baalah wadi ya Korr, Marsabit wateta uhaba wa maji, waitaka serekali ya kaunti kuwatengenezea visima.

Na JB Nateleng

Wakaazi wa eneo la Baalah Normads iliyoko Korr, eneobunge la Laisamis wamelalamikia kero la uhaba wa maji wakiitaka serekali ya kaunti na serekali kuu kuweza kuwatengenezea visima vya maji.

Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa eneo hilo, Rose Hosso ambaye pia ni mkazi wa eneo hilo amesema kuwa wamekumbwa na changamoto ya maji kwa muda sasa huku wakisafiri masafa marefu kusaka maji ambayo pia wakati mwingine inakuwa vigumu kupata.

Hosso ameelezea kuwa uhaba huu wa maji umeweza kuathiri pia elimu ya watoto katika eneo hilo huku akitoa wito kwa idara ya maji jimboni kuweza kuwasaidia katika kuchimba visima karibu na manyatta ili kuboresha hadhi ya elimu katika eneo hilo pamoja na kupunguzaa masafa marefu ambayo wakazi wanatembea kupata maji.

Subscribe to eNewsletter