Understanding Elavil: Uses, Benefits, and Safety
December 26, 2024
NA ISAAC WAIHENYA
Sasa ni afueni kwa wananchi wa maeneo ya Korr na Kargi baada ya wizara ya elimu kutuma kitita cha shilingi milioni 50 kujenga shule ya Mary Ngoyoni Memorial school ili kupiga jeki elimu katika maeneo hayo.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Joseph Maki ni kuwa shule hiyo itajengwa katikati ya maeneo ya Kargi na Korr ili kutumika na wanafunzi kutoka maeneo hayo mawili.
Maki amesema kwamba mikakati yote imekamilika huku kilichosalia tu ni kuanza rasmni kwa ujenzi wa taasisi hiyo ya elimu.
Ametaja kwamba serekali iliridhia ombi la kujengwa kwa shule katika eneo hilo baada ya kilio cha wakaazi waliokuwa wanalazimika kusafiri mbali ili kuwapa wanao elimu.