Local Bulletins

WIZARA YA AFYA KAUNTI YA MARSABIT YAONGEZEWA SHILLINGI MILIONI 50 KWENYE BAJETI YA MWAKA HUU.

 Na Isaac waihenya

Ni afueni kwa wizara ya afya kaunti ya Marsabit baada ya bunge la kaunti kuamua kuongeza shillingi milioni 50 kwa idara ya Afya. Haya ni kwa mujibu wa Christopher Ogom ambaye ni mwanachama wa kamati ya afya katika bunge la kaunti na pia mbunge wa eneo la Kargi.

Ogom ameelezea kuwa kumekuwepo na changamoto katika idara ya afya ambayo ilielezea idara hiyo kuwa kuna uhaba wa madawa lakini kwa sasa, serekali inatazamia kulipa deni la shillingi million 35 kwa almashauri ya kusambaza dawa nchini KEMSA ili kuhakikisha kuwa idara hiyo imepata dawa za kutosha.

Ogom ameeleza kuwa Watahakikisha kwamba fedha za kutosha zinatengewa idara ya Afya ili kuhakikisha kuwa vifaa vya hospitali vinapatikana. Pia kamati yake itaendeleza ziara za kufanya ukaguzi katika hospitali zingine za kaunti ili kuhakikisha kuwa wameboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Marsabit.

 Adhi Bino  ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya afya katika bunge la Kaunti amesema kuwa watazidi kushawishi viongozi wote kuweza kuwekeza katika kuboresha idara ya afya kwani ndio uti wa mgongo wa kaunti.

Mkurugenzi wa Afya katika kaunti ya Marsabit Boru amepongeza hatua ya kuongezewa kwa fedha hizo akisema kuwa itasaidia katika kuboresha afya katika kaunti ya Marsabit.

Subscribe to eNewsletter