Local Bulletins

SERIKALI YAAHIDI KUWEKA MIKAKATI YA KUBORESHA TAA ZA MJINI MARSABIT- WAZIRI WA ARDHI AMINA CHALA

NA LELO WAKO

Waziri wa   Ardhi, Ukuaji wa mji na Kawi katika kaunti ya Marsabit, Amina Chala amesema kuwa idara ya ukuaji wa mji itaweka mikakati kuweka taa za barabarani mjini Marsabit ili kuimarisha usalama na kusaidia wanabiashara kuendeleza biashara hata nyakati za usiku.

Akizungumzia hitilafu iliyo ofisini mwake waziri Amina ameeleza kuwa tatizo hilo linalokumba wakaazi kwa muda mrefu limesababishwa  na hatua ya  mwakandarasi (EP Global) kutokabidhi mradi huo kwa serikali mwaka wa 2017 kutokana kesi ya deni la milioni 36 inayodai kaunti tatizo analosema limerejesha nyuma mchakato huo.

Anasema wanafanya  juhudi kutatua suala hilo ikiwemo kutumia njia ya mazungumzo na  kuelewana na wanakandarasi huyo ili kukabidhi majukumu ya kuweka taa hizo wizara yake.

Hata hivyo Amina amesema kuwa  idara yake imezindua taa kubwa za ‘Flood Lights’ katika maeneo  mbalimbali ikiwemo  mjini Marsabit hatua anayosema kuwa imewezesha wanabiashara mjini kufanya shughuli zao hata wakati wa usiku.

Vile vile, Amina Chala akizungumzia mipango ya usoni, ameeleza kuwa  watashirikiana na mashirika mbalimbali ili waweze kuwekeza mradi wa  taa za barabarani mjini katika mwaka huu.

Subscribe to eNewsletter