IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Na Caroline Waforo
Waziri wa usalama wa kitaifa Kithure Kindiki ametahadharisha vyombo vya habari nchini dhidi ya kueneza maneno ya uchochezi wa umma.
Waziri alizungumza katika uzinduzi wa nne wa mpango wastani ambao unajumuisha kipindi cha mwaka 2023-2027, kikao cha kuhusisha umma na ufafanuzi wa programu ya maendeleo katika kaunti ya Marsabit, hafla iliyoandaliwa katika ukumbi wa kanisa katoliki.
Haya yanajiri wakati ambapo baadhi ya vyombo vya habari jimboni Marsabit vimekuwa vikionywa dhidi ya uchochezi.
Kindiki pia aliwaonya wanasiasa walio na nia ya kueneza uchochezi wa kikabila humu jimboni Marsabit.
Na huku kaunti ya Marsabit ikiendelea kushuhudia utulivu na Amani kwa muda sasa waziri Kindiki amesema kuwa bado kunazo changamoto za kiusalama huku akisema kuwa serikali ya rais William Ruto itahakikisha kuwa inatokomeza utovu wa usalama jimboni kikamilifu.
Kadhalika Kindiki amedokeza kuwa Serikali kupitia wizara yake ya usalama wa ndani ina mpango wa kuongeza maafisa wa akiba NPR ili kusaidia maafisa wa usalama katika kudumisha Amani jimboni.