NDOTTO WARRIORS WATWA UBINGWAWA TAJI LA AHMED KURA TOURNAMENT MWAKA 2024…
December 18, 2024
Wazee wa baraza la jamii ya Gabra-Yaa wameapa kuungana kupigania umoja wa jamii kabla ya uchaguzi.
Wakizungumza wakati wa mkutano wa siku mbili uliowakutanisha wazee kutoka yaa Galbo, Yaa Algana, Yaa Sharbana, Yaa Garr na Yaa Odhol wazee wa baraza hilo wamesihi wanajamii kuungana kwa pamoja kwa minajili ya maendeleo ya jamii.
Menyekiti wa shirika la Tokuma Aaada Trust ambalo lilifadhili mkutano huo Molu Kala Galgallo amesema kando na suala la utamaduni, wanalenga pia kuendelea kuhamasisha jamii kuhusu haja ya kuishi kwa amani na jamii nyingine jirani.
Aidha viongozi waliozungumza katika mkutano huo wamekubaliana kuwa jamii hiyo imeshindwa kutatua changamoto nyingi kwa sababu ya ukosefu wa maelewano.
Wametaja mtindo wa watu mashuhuri kuingilia majukumu ya baraza hilo kama vile mchakato wa kutawaza viongozi kuwa kinyume na mila za jamii.
Suala ambalo limefanya baraza hilo kuonekana kwamba hawana uwezo wa kusuluhisha masuala ya jamii, jambo ambalo wazee hao wameahidi kurekebisha ili jamii iweze kupata mwelekeo unaofaa kisiasa.
Mkutano mwengine wa baraza hilo umepangwa kufanyika mwaka ujao mwezi machi kijiji cha Yaa Algana ukitarajiwa kuhusisha wazee pekee.