Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Baadhi a desturi ambayo wazazi wanatumia kuwatibu watoto waliochelewa kutembea imetajwa kuathiri watoto wengi na hata kuwaletea shida za kimwili.
Kulingana na Waqo Huqa ambaye ni daktari anayeshughulikia ulemavu watoto amesema wazazi wengi hutumia njia ya kitamaduni ambazo zinaathiri maisha ya watoto na hata kuwasababishia ulemavu.
Huqa akizungumzia mila hizo, amesema kati ya njia hizo ni kama vile kukata watoto paja, kung’oa meno, kuchanja mgongo.
Aidha amesema kuwa baadhi ya desturi hizo zinaweza kuleta uharibifu ya misuli na kusababisha kufuja damu hatua inayoweza kuchangia watoto kufa.
Vile vile amesema kuchelewa kwa watoto kunachangiwa kosefu wa lishe bora na baadhi ya shida nyingine mwilini.
Hata hivyo Huqa amewarai wazazi kutembelea hospitali ili wapate ushauri ya madaktari.