Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Watu watano wanadaiwa kufariki kutokana na maporomoko ya migodi ya Hilo eneo la Dabel Kaunti ndogo ya Moyale kaunti hii ya Marsabit
Akithibitisha tukio hilo,chifu wa Dabel Ibrahim Dube amehoji kuwa watu watano wamethibitishwa kufariki na idadi ya watu isiojulikana ikiwa imefunikwa na Mchanga Katika migodi ya Hilo.
Tukio hilo lilitokea Jumatatu jioni. Wakuu wa usalama kaunti ya Marsabit wamekosoa kuzungumzia tukio licha ya meza yetu ya habari kutafuta kauli zao.
Hali hiyo inajiri hata licha ya serikali kutangaza kufungwa kwa migodi hiyo ya dhahabu.
Licha ya amri iliyotolewa na aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani ambaye kwa sasa ni Naibu Rais Prof Kindiki Kithure visa vya watu kufariki kutokana na maporomoko ya migodi ya Hillo vinazidi kushuhudiwa mara kwa mara