Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya haki za binadamu duniani watu wanaoishi na ulemavu katika kaunti ya Marsabit wamelalama kuwa bado wanazidi kudhulumiwa kijinsia huku vingi vya visa hivyo vikikosa kuripotiwa.
Wakizungumza na Shajara ya Radio Jangwani wakiongozwa na Halima Osman, watu hao wanaoishi na ulemavu wametaja kwamba ipo hoja ya serekali kukaza Kamba katika kukabiliana na visa vya dhulma za kijinsia haswa kwa walemavu.
Aidha wamelitaja swala la kukosa mtafsiri katika tasisi muhimu ikiwemo hospitali kama jambo lingine linalolemaza haki zao.
Hata hivyo mkurugenzi wa idara ya huduma za jamii kaunti ya Marsabit Galgallo Okotu ametaja kwamba serekali ya kaunti imejiza titi kuhakikisha kwamba inawainua watu wanaoishi na ulemavu kwa kuwapa huduma na misaada mbalimbali.
Vilevile Okotu amewataka wananchi kutowaficha watu wanaoishi na ulemavu na badala yake kuhakikisha kwamba wamepata haki ya elimu ili kujifaidi katika maisha yao ya usoni.