Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
NA GRACE GUMATO
Shughuli ya kuhamasisha jamii wanaoishi karibu na msitu na kuisajili kamati mpya itakayosimamia jamii katika maswala ya misitu inaendelea katika lokesheni mbali mbali katika eneo bunge la Saku katika kaunti ya Marsabit.
Kulingana na John Wako ambaye ni mwakilishi wa jamii katika uhifadhi wa misitu ni kuwa uchaguzi wa kamati mpya inaendelea katika lokesheni 11 na kwa sasa ni lokesheni mbili tu haijafikiwa ambayo ni Dirib na Monajida ambayo ni Mountain, Nagayo, Jirime Na Dakabaricha akisema kuwa kamati hiyo itasaidia wanachni kutoa mapendekezo yao kuhusu utumizi wa misitu.
Aidha wako amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kujisajili kama wanachama wa muungano wa msitu wa kijamii (Community Forest Association) akitaja faida hizo ikiwemo kufaidika na maji na pia kupewa kibali cha kukusanya dawa za kinyeji katika msitu.
Hata hivyo wako amerai jamii wanaoshi karibu na msitu kutowapeleka mifugo wao kwenye msitu akisema kuwa kwa sasa nyasi zinapatikana kwa urahisi nje ya msitu.