Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
BY JOHN BOSCO NATELENG
Mwanachama wa kamati kuu ya chama cha kisiasa cha National Vision Party (NVP), Harrison Mugo, anasema kuwa suala la muguka linahitaji kuzingatiwa kwa undani ili kukwepa migogoro inayoweza kuzuka kati ya wauzaji wa bidhaa hiyo na serikali.
Akizungumza katika mahojiano, Mugo amesema kuwa ni jukumu la wataalamu husika kutoa mwongozo dhabiti kuhusu matumizi ya muguka, badala ya viongozi kuchukua maamuzi ya kufanya marufuku.
Ameeleza kuwa hii inaweza kuwa ni hatua ya baadhi ya wanasiasa kujipatia umaarufu.Hata hivyo, Mugo amewajuliliza wanasiasa kuyapima maneno yao kwa nia ya kuboresha nchi, kwani wale wanaoumiwa zaidi ni wananchi wenyewe ambao wanatarajia mema kutoka kwao.