Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
Na Samuel Kosgei
Muungano wa wataalam na wasomi kutoka jamii ya Gabra kaunti hii ya Marsabit hii leo wameandaa mkutano ulionuiwa kuunganisha jamii hiyo baada ya viongozi wao kuchukua mwelekeo tofauti wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Akizungumza katika hafla hiyo mwenyekiti wa muungano huo wa Gabaro Professional Assocciation, Prof. Dulacha Barako amesisitiza umuhimu wa jamii hiyo kuwa na umoja na kujipanga upya kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027.
Amesema kuwa muungano huo wa wasomi umejikusanya pamoja ili kusukuma ajenda ya jamii mbele bila kutegemea viongozi wanasiasa anaosema kuwa kwa muda wamekuwa wakigawanya jamii kwa malengo yao ya kibinafsi.
Profesa Dulacha pia ametaja kusikitishwa na ukosefu wa umoja wa jamii mwaka wa 2022 suala lililochangia wao kupoteza kiti cha ugavana katika kaunti hii ya Marsabit.
Amewataka wanasiasa kuacha kugawanya jamii kwa manufaa yao binafsi.