Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Mkurugenzi wa elimu kaunti ya Marsabit Peter Magiri, amesema kuwa serikali kupitia wizara ya elimu itawapa fursa Wasichana waliopata Watoto wakiwa shuleni fursa ya kuendelea na masomo yao ili kutimiza ndoto zao siku za usoni.
Akizungumza kwenye mkao wa siku ya mwisho ya kufuzu kwa Wasichana 200 kwenye programu ya gaddis gamme mjini Marsabit, Magiri amesema kuwa idara ya elimu haikurekodi kisa chochote cha Wasichana kufanya mtihani katika hospitali kutokana na kuzalia hospitali.s
Wazazi wa wasichana walionufaika na mafunzo hayo ya Watoto Wasichana wamesema kuwa programu hiyo haikuwa na ubaguzi na imesaidia kupunguza dhulma za kijinsia haswa kwa wasichana
Wakati uo huo Wasichana walioshiriki elimu hiyo wamesema wamenufaika na mafunzo hayo na pia kushukuru mkewe gavana wa Marsabit Alamitu Guyo kwa kuanzisha programu hiyo ya Gaddis Gamme.