Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Watu watatu walionaswa hapo jana na bunduki haramu aina ya AK47 kule Manyatta Daaba Lokesheni ya Jirime kaunti ya Marsabit wamefikishwa mahakamani Jumanne mbele ya hakimu mwandamizi Simon Arome.
Watatu hao wameshtakiwa kwa makosa mawili kila moja yanayofungamana na umiliki wa silaha hatari kinyume na sheria pamoja na risasi.
Mshukiwa wa kwanza Sora Boru Galma ameshtakiwa Kwa kumiliki bunduki pamoja na risasi 30, mshukiwa wa pili Kadiro Osman Ali pia ameshtakiwa kwa kumiliki bunduki pamoja na risasi 60 huku naye Miyo Qanchora Jirmo aliye na chini ya umri ya miaka 18 akishtakiwa Kwa kumiliki bunduki vile vile risasi 30.
Mshukiwa wa kwanza na wa pili wamepewa bondi ya shillingi millioni 2 huku mshukiwa wa tatu akiwaachiliwa kwa Bondi ya shillingi 300,000 au pesa taslimu shilingi laki moja.
Kesi hiyo itatajwa tarehe 19 mwezi huu wa Disemba.