Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Lelo Wako
Wanawake wanafaa kuaminiwa katika uongozi nchini Kenya bila kubaguliwa kijinsia.
Hiyo ni kauli yake, Sadia Araru ambaye ni mwakilishi wadi mteule katika bunge la kaunti ya Marsabit akieleza kuwa uteuzi wake Soipan Tuya kama waziri wa ulinzi unamfaa.
Katika kauli yake, Sadia amekiri kuwa mwanamke pia ana uwezo wa kuongoza wizara yoyote kama vile mwanaume. Amekashifu kauli ya baadhi ya wananchi kuwa wanawake hawana uwezo wa kutosha kufanya kazi zingine.
Aidha, Sadia amelalamikia tatizo la wanawake kukandamizwa na mila za jamii katika kaunti ya Marsabit akisema wanawake wanapuuzwa na kuonekana kama Watoto katika jamii.
Vile vile Sadia amewahimiza wakaazi wa kaunti ya Marsabit kuweza kukumbatia uongozi wa wanawake huku akitoa ombi kwao kuzingatia usawa wa kinjinsia katika kuchagua viongozi.