Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Huku siku 16 za uanaharakati kupinga vita vya dhulma za kijinsia haswa dhidi ya wanawake ikikamilika hii leo wanawake na wasichana kaunti ya Marsabit wamejitokeza kukashifu wanawake kunyanyaswa na wanaume.
Wakizungumza na Shajara ya Radio Jangwani wakati wa matembezi mjini Marsabit, wanawake hao wamesema kuwa wanawake wengi wanapoteza maisha yao kila mwaka nchini jambo ambalo wametaja kama la kusikitisha.
Wakati uo huo wanawake hao wamewarai wanaume kutochukua hatua mikononi mwao wanakapokosana na wake wao badala yake kufuata njia sahihi za kusuluhisha migogoro nyumbani.
Huku wakishukuru shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Right Defenders kwa kuwafadili wao, wanawake hao wametoa wito kwa wanaume kuwasikiza kwa kuwapa sikio wanapopitia matatizo nyumbani.