Serekali yatakiwa kutoa hamasa kwa jamii kuhusiana na ongezeko la visa vya mauaji ya wanawake na wasichana nchini.
January 28, 2025
Wakaazi katika kaunti ya Marsabit wamehimizwa kutotupa takataka ovyo ovyo bila idhini ya manispaa ya Marsabit. Ni hamasisho ambayo imetolewa na mkurugenzi katika manispaa ya mji wa Marsabit Boru Golicha.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee golicha amesema wakati huu ambao msimu ya mvua unatarajiwa, kutupa taka ovyo ovyo bila kukaguliwa na idara ya afya umma na wamazingira ni hatari kwa wakaazi na hata mifugo.
Golicha ametoa tahadhari kwa hoteli zinazotupa takataka kiholela bila idhini kutoka afisi ya manispaa kuwa watachukukiliwa hatua ya kisheria. Kuligana na mkurugenzi huyo ni kuwa kuna aina nyingi ya takataka ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu hivyo ni muhimu watu kuwa na stakabadhi au idhini ili aina ya taka ibainike.
Aidha Golicha amerai wakaazi ambao ni washikadau kuripoti wanapoona mambo ambayo siyo ya kawaida ili waotupa takataka ovyo ovyo wachukuliwe hatua kali za kisheria.