Local Bulletins

WANAOTEGEMEA DHAHABU WAOMBWA KUVUMILIA HADI MARUFUKU ILIYOWEKWA NA SERIKALI ITAKAPOKAMILIKA.

Na Samuel Kosgei

NAIBU kamishna wa kaunti ndogo ya Moyale Benedict Munywoki amekariri umuhimu wananchi wa eneo la Dabel kunakochimbwa dhahabu kuzidi kuvumilia hadi marufuku iliyowekwa na serikali itakapokamilika.

Munywoki akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu amesema kuwa iwapo wananchi wataepuka kufika eneo la mgodi wa dhahabu basi maafa kama yaliyoshuhudiwa mwezi jana hayawezi yakashuhudiwa tena.

Kiongozi huyo wa usalama amekariri kuwa bado marufuku hiyo ingalipo na kuonya wanaojificha kwenda kwenye machimbo hayo akisema kuwa watakamatwa na maafisa wa usalama ambao wamezidi kukita kambi katika eneo hilo.

Kauli yake DCC Munywoki inajiri siku chache baada ya waziri wa usalama wa kitaifa Kithure Kindiki kuzuru kaunti ya Marsabit na kukariri haja ya wananchi kuepuka eneo hilo hadi mikakati mwafaka itakapowekwa na wizara yake ikishirikiana na wizara ya madini.

Subscribe to eNewsletter