Local Bulletins

WANAMARSABIT WATOA MAONI KINZANI KUHUSIANA NA MADAI YA COG KUWA SERIKALI KUU INAPANIA KUNYAKUA SEKTA YA AFYA.

Na Ebinet Apiyo

Huku zikisalia siku chache tu kabla ya Bajeti Mpya kusomwa na Baraza la Magavana (CoG) kushutumu serikali kuu kwa kula njama ya kupokonya kaunti sekta ya afya, baadhi ya wakaazi wa mji wa marsabit wameunga mkono nia hiyo wakidai kaunti zimeshindwa kuendesha sekta ya afya.

Hata hivyo baadhi ya wakaazi pia wamedai kuwa kaunti hazijashindwa kudhibiti sekta ya afya ni vile tu serikali kuu imeshindwa kutuma mgao wa pesa kwa serikali za kaunti hivyo kulemaza juhudi zao.

Siku za hivi karibuni serikali ya kitaifa imeonekana kutamani kurejeshewa sekta ya afya huku ikisawiri majimbo kama yiliyoshindwa kusimamia idara hiyo muhimu.

Subscribe to eNewsletter