Local Bulletins

WALIMU WAKUU JIMBONI MARSABIT WATAKIWA KUWA MAKINI ILI KUZIA VISA VYA MIKASA YA MOTO.

Na Caroline Waforo,

 Walimu wakuu humu jimboni Marsabit wametakiwa kuwa makini ili kuzia visa vya mikasa ya moto.

Ni tahadhari ambayo imetolewa na kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau ambaye amezungumza na meza ya Radio Jangwani afisini mwake.

Kamishna Kamau anasema kuwa iwapo walimu wakuu watahakikisha kuwa wanakabiliana na visa vyovyote vya utovu wa nidhamu kutoka kwa wanafunzi kwa mapema basi mikasa ya moto itaweza kuepukika.

Kauli yake inajiri huku mikasa moto katika shule mbalimbali nchini ikiongezeka katika siku za hivi maajuzi.

Alhamisi wiki jana moto uliteketeza bweni la shule ya Hillside Endarasha kaunti ya Nyeri na kusababisha maafa ya wanafunzi 21 huku 17 hawajulikani waliko hadi kufikia sasa.

Aidha usiku wa Jumamosi bweni la shule ya wasichana ya Isiolo liliteketea na kusababisha uharibu wa mali.

Usiku wa jana shule Njia boys iliyoko Maua kaunti ya Meru iliteketea japo hakuna majeruhi.

Asubuhi ya leo bweni la shule ya Ortum Boys iliyoko Kapenguria kaunti ya Wwest Pokot liliteketea. Hakuna aliyejeruhiwa katika mkasa huo.

Subscribe to eNewsletter