Local Bulletins

WAKAAZI WA MARSABIT WATOA MAONI TOFAUTI KUHUSIANA NA MAPENDEKEZO YA KUUNDWA KWA OFISI YA KIONGOZI WA UPINZANI.

Na Talaso Huka

Wakaazi wa kaunti ya Marsabit wametoa hisia mseto kuhusu pendekezo la kuundwa kwa afisi rasmi ya kiongozi wa upinzani.

Baadhi ya waliozungumza na Radio Jangwani wameunga mkono pendekezo hilo wakisema kuwa kuundwa  kwa ofisi rasmi ya upinzani itasaidia katika kuwajibisha serikali

Hata hivyo mmoja wa mkaazi ameonekana kupinga pendekezo  hilo akidai kuwa itaongeza mzigo kwa mlipa ushuru ambao tayari wanendelea kukabiliana na gharama ya juu ya maisha.

Akizungumza hiyo jana katika kaunti ya Homabay wakati wa ziara ya rais William ruto kule Luo Nyanza, mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed alidokeza kuwa  kwa ushirikiano na kiongozi wa walio wengi katika bunge la kitaifa Kimani Ichungwa wanaandaa mswada unaopendekeza kuundwa kwa afisi hiyo.

Itakumbukwa kuwa hii ilikuwa mojawapo ya mapendekezo katika ripoti ya pamoja ya NADCO.

Subscribe to eNewsletter