Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Wakaazi wa Marsabit watoa hisia zao kuhusiana na mzozo katika ya bunge na mahakama unaohusu IEBC…
Baada ya kutibuka kwa mzozo kati ya Bunge na Mahakama kuhusu kucheleweshwa kwa uteuzi wa makamishina wa tume huru ya uchaguzi na mipaka(IEBC), wakaazi katika kaunti ya Marsabit wametoa hisia zao kuhusu suala hilo.
Baadhi ya waliozungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, wamesema kuwa ni Rais Ruto ndiye anayehusika na kuchelewesha kwa uchaguzi wa wajumbe wa IEBC.
Aidha, wengine wao wamesema kuwa Mahakama imefeli katika kazi yake ya kuwalinda wananchi wakidai kuwa mahakama inadhibitiwa na Rais Ruto.
Hata hivyo, wametoa rai kwa Ruto kuharakisha mchakato huo wa kuwateua makamishina wa IEBC kwani ndiye mwenye uwezo huku wakipendekeza viongozi wa kidini kutokimywa na badala yake washirikiane kwa pamoja kuhakikisha kwamba swala hilo limetatuliwa.