Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
Na Ebinet Apiyo,
Baada ya kinara wa upinzani nchini Raila Odinga kuonekana kufanya kazi na serekali na baadhi ya wanachama wa ODM kuteuliwa kama mawaziri, wakaazi wa kaunti ya Marsabit wametoa hisia zao kuhusiana na iwapo kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka anatosha kushikilia wadhifa wa kinara wa upinzani nchini.
Baadhi ya waliozungumza na idhaa hii wamelitia shaka ufaafu wa Kalonzo kuwa kinara wa upinzani wakisema kwamba hana ushawishi wakutosha hata katika eneo anakotoka.
Wengine wao wamelalamikia kile wamekitaja kuwa ni ukosefu wa msimamo dhabiti katika kushughulikia mambo mbalimbali.
Aidha baadhi yao wamemtaja Kalonzo kama mtu pekee aliyesalia na ambaye anauwezo wa kushikilia wadhifa huo haswa kuzingatia viongozi wengine katika muungano wa Azimio.