Local Bulletins

Wakaazi wa Marsabit watoa hisia kinzani kuhusiana na utafiti uliomuorodhesha gavana Mohamed Ali kati ya magavana 10 ambao hawajafanya maendeleo.

Wakaazi wa Marsabit watoa hisia kinzani kuhusiana na utafiti uliomuorodhesha gavana Mohamed Ali kati ya magavana 10 ambao hawajafanya maendeleo.

Baadhi ya wakaazi katika kaunti ya Marsabit wameutaja utafiti wa hivi maajuzi uliomuorodhesha gavana wa kaunti ya Marsabit Mohamed Muhamud Ali katika orodha ya magavana kumi ambao hawajafanya maendeleo hapa nchini kama usio wa kweli.

Wailiozungumza na idhaa hii wameutaja utafiti huo kama maonevu kwa gavana kwani kuna miradi taajika kama vile chuo cha mafunzo ya matibabu KMTC,sawa na vyuo vingine vya anuai ambavyo vimekamilishwa chini ya uongozi wa gavana Ali.

Aidha baadhi yao wamelitaja swala la usalama kama jambo la kujivunia kwani huchangia pakubwa katika kuhakikisha kwamba kuna maendeleo hapa jimboni.

Hata hivyo wengine wao wameutaja utafiti huo kama hali halisi ilivyo katika maeneo mbalimbali hapa jimboni huku wakikariri kuwa gavana Ali pia hajatekeleza baadhi ya miradi aliyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita wa mwaka 2022.

Subscribe to eNewsletter