Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Caroline Waforo
Huku serikali ikiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu uhalali na muda wa matumizi wa vitambulisho vya kidigitali Maisha Card, wakaazi wa Kaunti ya Marsabit wametakiwa kupuuza propaganda zinazoenezwa kuhusiana na uhalali na muda wa vitambulisho hivyo.
Akizungumza na Shajara afisini mwake afisa wa usajili jimboni Marsabit Michael Oduor ameweka bayana sababu kuu ya hitaji la watu walio na Maisha Card kubadilisha vitambulisho vyao kila baada ya miaka kumi bila kuhitaji usajili mpya wa kidijitali.
Oduor ameeleza kuwa kila mtu atahitajika kuwa na kitambulisho ila serikali haitamlazimisha Wakenya kuwa na Maisha Card.
Aidha ameeleza umuhimu wa Wakenya kukumbatia Maisha Card ikilinganishwa na vitambulisho vya kawaida.
Kwa Sasa anayewasilisha ombi la kuwa na kitambulisho kwa mara ya kwanza atapokezwa maisha card Kwa shillingi 300 malipo yatakayolipwa kupitia mfumo wa E CITIZEN.
Iwapo utapoteza kitambulisho chako itakugharimu shilingi 1,000 kupata kitambulisho kipya cha maisha card sawa na wanaotaka kubadilisha deta zilizo kwenye kitambulisho.
Na iwapo unacho kitambulisho cha kawaida na unataka kupata maisha card pia itakugharimu shilingi 1000.
Zoezi la kuwapa Wakenya Maisha Card ulioanzishwa Februari 23 mwaka huu huku jumla ya Wakenya 972,630