Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Wakaazi wa Marsabit watakiwa kuhakikisha kwamba wasichana walio na umri wa miaka 9-14 wamepokea chanjo ya HPV.
Na Grace Gumato
Wito umetolewa kwa wakaazi wa kaunti ya Marsabit kuwapeleka wasichana wao walio na umri wa miaka 9-14 katika vituo vya afya kupokea chanjo ya HPV.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, Dkt Eric Simiyu alisema kuwa chanjo hiyo inasaidia kuzuia Saratani ya njia ya uzazi (Cervical Cancer) kwa wasichana, akisema kuwa wanawake walio na umri zaidi ya 50 wako katika hatari ya kupata saratani hiyo.
Aidha dkt Simiyu alivitaja visababishi vyake kama ifutavyo: Kuwa na wapenzi wengi wa ngono, magonjwa ya zinaa, ugonjwa wa upungufu wa kinga mwilini kama vile Ukimwi.
Amewashauri wanawake kutembelea vituo vya afay kufanyiwa uchunguzi wa saratani.